Winga wa klabu ya Manchester City na timuu ya taifa ya Uingereza Jack Grealish amezua gumzo kubwa katika sherehe za ubingwa wa mskombe matatu ambao wameipata klabu yake.
Jack Grealish amekua na shangwe sana kwenye kikosi kizima cha Manchester City baada ya kutwaa taji la ligi ya mabingwa ulaya siku ya humamosi jijini Instabul nchini Uturuki, Huku akiripotiwa kulewa sana katika kushangilia makombe hayo.Winga huyo amekua akionekana katika video nyingi akiwa amelewa na hii imemfanya kuibua gumzo zaidi mitandaoni kutokana na video zake kuendelea kusambaa na mpaka sasa winga huyo anaendelea kuzungumzwa zaidi kutokana na ambacho kilichotokea.
Grealish anaripotiwa alihitajika kuitiwa kiti cha kukaa kutokana na kuzdiwa kutokana na ulevi wa kupindukia wakati wa sherehe za ubingwa zikiendelea, Lakini pia kua picha inaonekana ameshikwa na mchezaji mwenzake Kyle Walker akiwa pia amelewa.Pamoja na yote yaliyotokea kwa upande wa Jack Grealish lakini mchezaji huyo raia wa kimataifa wa Uingereza ni wazi amekua na msimu bora sana ndani ya kikosi cha Manchester City na kua moja ya mchezaji muhimu chini ya kocha Pep Guardiola.