Manchester United Yamuwinda Nyota wa Palace

Klabu ya Manchester United inamuwinda winga wa klabu ya Crystal Palace nyota wa kimataifa wa Uingereza Eberechi Eze katika kipichi hichi cha majira ya joto.

Manchester United inataarifiwa kua inamuwinda Eberechi Eze wa Crystal Palace kwajili ya kuboresha timu hiyo kuelekea kampeni za msimu ujao wa mwaka 2023/24 na kocha Ten Hag anaona kama kiungo huyo anaweza kua nyongeza nzuri ndani ya timu hiyo.manchester unitedEberechi Eze amekua na msimu bora ndani ya Crystal Palace na kua miongoni mwa wachezaji muhimu wa timu hiyo kando ya Wilfred Zaha pamoja na Oliseh na klabu mbalimbali zimeanza kumtolea macho wakiwemo mashetani wekundu.

Manchester United mpaka sasa haijafanikiwa kukamilisha usajili wa mchezaji yeyote kuelekea msimu ujao, Hivo inawezekana Eze akawa usajili wa mapema ndani ya timu hiyo kama watakua makini kwani mchezaji huyo hana gharama kubwa.manchester unitedTaarifa zinaeleza kua kocha wa klabu ya Manchester United anavutiwa na Eberechi Eze kwani anaweza kutumika katika nafasi tofauti uwanjani kwani mchezaji huyo anaweza kutumika kama kiungo mshambuliaji lakini vilevile anaweza kutokea pembeni kama winga.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.