Klabu ya Manchester United sasa imemgeukia mshambuliaji wa mabingwa wa Italia raia wa kimataifa wa Nigeria Victor Osimhen baada ya kuona ugumu kwenye dili la Harry Kane.
Manchester United walikua wamemueka Harry Kane kama chaguo lao la kwanza katika nafasi ya ushambuliaji kwenye majira haya ya joto, Lakini mpaka sasa dili hilo linaonekana kutokuendelea kutokana na ugumu ambao upo wa kibiashara baina ya klabu hiyo na Mwenyekiti wa klabu ya Tottenham Daniel Levy.
Victor Osimhen anaonekana kua chaguo mbadala kwasasa baada ya dili la Kane kusuasua ambapo mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Nigeria ana namba nzuri sana kwa msimu uliomalizika ambapo pia amemaliza kama mfungaji bora wa ligi kuu ya Italia.
Manchester United wamekumbana na upinzani mkali kutoka kwa bosi wa klabu ya Tottenham ambae ni wazi anaonekana hataki kumuuza Harry Kane kwa klabu hiyo jambo ambalo limewafanya klabu hiyo kufikiria mbadala wa mchezaji mwingine ambaye ni Victor Osimhen.
Klabu ya Manchester United imetahadharishwa pia kwa klabu ya Napoli majadiliano hayatakua mepesi kwani rais wa klabu hiyo Auriello de Laurentiis ni miongoni mwa mabosi watata kama Daniel Levy wa Tottenham.

