Mshambuliaji wa Yanga raia wa kimataifa wa Congo Fiston Mayele atatimka ndani ya klabu hiyo muda wowote kuanzia sasa na ataelekea klabu ya Pyramids nchini Misri.
Mchezaji Fiston Mayele inaelezwa aliandika barua ya kuomba kuondoka ndani ya klabu ya Yanga baada ya fainali ya michuano ya kombe la shirikisho, Baada ya hapo Yanga walikaa nae vikao kadhaa kwajili ya kutaka kumbakiza lakini haikuwezekana.
Yanga walihitaji kuhakikisha wanambakiza mchezaji huyo kwa kumboreshea mshahara wake lakini kila jitihada walizozifanya klabu hiyo hazikufanikiwa, Hivo klabu hiyo wamefikia hatua ya kukubali kumuachia mchezaji huyo.
Mayele alikua ana mkataba na Yanga wa mwaka mmoja mpaka mwaka 2024 hivo klabu ya Yanga inaelezwa imefanya biashara nzuri na klabu ya Pyramids kutoka nchini Misri inakadiriwa wanaweza kuingiza kiasi cha Bilioni 2.
Klabu ya Yanga itatangaza muda wowote kuachana na mchezaji huyo na atajiunga na klabu hiyo ya Misri akitokea kwa mabingwa hao wa ligi kuu ya NBC, Mayele ataweka rekodi kua mchezaji aliyeuzwa kwa gharama zaidi ndani ya klabu ya Yanga.

