Klabu ya Manchester United ipo kwenye mchakato wa kumsajili kiungo wa klabu ya Bayern Munich raia wa kimataifa wa Ujerumani Leon Goretzka ndani ya dirisha hili.
Manchester United mpaka sasa imeshafanikiwa kusajili kiungo mmoja ambaye ni Mason Mount kutoka klabu ya Chelsea, Huku taarifa kutoka ndani ya klabu hiyo zikieleza kua wanahitaji kusajili kiungo mwingine ambapo Leon Goretzka yupo kwenye orodha.
Kiungo Leon Goretzka amekua mchezaji muhimu ndani ya klabu ya Bayern Munich kwa misimu kadhaa, Lakini mashetani hao wekundu wanavutiwa na uwezo wa mchezaji huyo na inaelezwa wanataka kutuma ofa ndani ya klabu ya Bayern Munich.
Manchester United licha ya kuonesha nia ya kutaka huduma ya kiungo huyo wa kimataifa wa Ujerumani, Lakini kocha wa klabu ya Bayern Munich amesema kua nyota huyo bado wanamuhitaji kwenye kikosi chao na bado ana mkataba na mabingwa hao wa Ujerumani.
Taarifa kutoka ndani ya klabu ya Manchester United zinaeleza kua klabu hiyo inafukuzia kwa karibu saini ya nyota huyo licha ya kufukuziwa na vilabu vingine kadhaa, Kwani kocha wa timu hiyo Ten Hag anaona ni kiungo anaeweza kuongeza kitu kwenye kikosi chake.

