Klabu ya Manchester United wameanza maandalizi ya msimu mpya vizuri baada ya kufanikiwa kupata ushindi wa mabao mawili kwa bila dhidi ya Leeds United katika mchezo uliopigwa nchini Norway leo.
Manchester United ambayo ilianza na wachezaji wa timu ya wakubwa saba huku wachezaji wanne wakiwa wanatoka timu ya vijana ya klabu hiyo ambapo walipata fursa ya kuanza mchezo huo uliochezwa jioni ya leo.
Mchezo huo huo kipindi cha kwanza ulionekana kua upande wa Man United na kutawala zaidi mcheza, Lakini mpaka timu zinakwenda mapumziko hawakua wamepata nafasi ya kufungana na mchezo kwenda kwa sare ya bila kufungana.
Kipindi cha pili kilianza kwa mabadiliko makubwa ambapo kocha Ten Hag alibadilisha kikosi kizima na kuingiza wachezaji wa timu ya vijana tupu ambapo ndio walioweza kuipatia ushindi wa mabao mawili klabu ya Manchester United leo.
Mabao ya Emeran na Hugill ndio yaliisaidia klabu ya Manchester United kufungua vizuri maandalizi yao kuelekea msimu ujao, Lakini pia leo mchezaji mpya wa klabu hiyo Mason Mount alifanikiwa kucheza mchezo wake wa kwanza na klabu hiyo.

