Klabu ya Fulham italazimika kuingia vitani kuhakikisha inambakiza winga wa kimataifa wa Brazil Willian klabuni hapo baada ya mkataba wake kumalizika mwezi Juni mwaka huu.
Fulham wamejikuta wanaingia vitani na klabu ya Nottingham Forest pamoja na vilabu vya Saudia Arabia ambao pia wanahitaji saini ya winga huyo ambaye amemaliza mkataba na klabu hiyo katika dirisha hili na kwasasa yupo huru.
Willian sasa yupo kama mchezaji huru sokoni hivo vilabu hivo vinavyomuwania vinahitaji kuanza mazungumzo nae ili kuangalia maslahi yake yanagharimu kiasi gani wakiwemo waajiri wake ambao amewatumikia msimu uliomalizika.
Fulham pamoja na Nottingham wanatarajiwa kutuma ofa rasmi kwa Willian ambapo vilabu vya Saudia navyo vikiwa havipo nyuma, Lakini hakuna uamuzi wowote kutoka kwa mchezaji mpaka sasa huku maamuzi yakitarajiwa kutoka siku kadhaa mbele.
Willian ameitumikia klabu ya Fulham msimu uliomalizika kwa kiwango kikubwa ambapo walimpa mkataba wa mwaka mmoja, hivo baada ya kumaliza mkataba wake klabu hiyo imemuhitaji tena baada ya kuvutiwa na kiwango alichokionesha klabuni hapo.

