Klabu ya Fulham ambayo inaongozwa na Marco Silva imeondoka na alama tatu kibabe wakiwa ni wageni wa mchezo waliocheza jana dhidi ya Nottingham Forest huku wakitoka nyuma baada ya kufungwa bao moja kwa bila mpaka kumalizika kwa kipindi cha kwanza.

 

Fulham Yapata Alama 3 Kibabe

Baada ya kurejea kwa kipindi cha pili na Fulham kufanya mabadiliko, ndipo wakanza kupata mabao ambao dakika ya 54 walisawazisha bao na baadae kuongeza mabao mawili huku mabao yote matatu yakifungwa ndani ya dakika 7 tuu huku Willian akitoa assist yake ya kwanza.

Huu ulikuwa ni mchezo wa tano mfululizo wa ligi kuu ya England kati ya timu mbili zilizopanda daraja kushinda ugenini, Ikiwa ni muda mrefu zaidi katika historia ya ligi kuu ya Uingereza. Fulham walishinda mchezo wa Premier League wakiwa wakiwa nyuma kwa muda wa mapumziko kwa mara ya kwanza tangu April 2009 dhidi ya Man City, wakitoa sare mara tisa na kupoteza 49 zaidi kati yao kutoka nafasi kama hiyo.

 

Fulham Yapata Alama 3 Kibabe

Nottingham Forest wameshinda mechi nne mfululizo za Premier League kwa mara ya kwanza tangu walipopoteza mara sita mwezi Agosti/Septemba 1992. Baada ya ushindi huo wa jana Fulham amesogea mpaka nafasi ya 6 katika msimamo huku akiwa na alama 11 huku akishinda mechi tatu, sare 2, na kupoteza mara 2. Huku Nottingham kupoteza mchezo wao wa jana wanazidi kudidimia chini ya msimamo wakiwa nafasi ya 19.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa