FIFA imethibitisha kukataa rufaa ya Chile na Peru ya kuiondoa Ecuador kushiriki michuano ya Kombe la Dunia kwa kumchezesha mchezaji asiyestahili. Michuano hiyo inatarajia kufanyika huko Qatar mwezi Novemba mwaka huu.

 

FIFA Yaisamehe Chile na Peru

Hapo mwanzo iliripotiwa kuwa Ecuador itakuwa hatarini kuondolewa katika michuano ya Kombe la Dunia la mwaka 2022 kutokana na utata wa nyaraka za mchezaji wake, Byron Castillo ambapo almedaiwa kuwa ni raia wa Colombia.

inasemekana kuwa uchunguzi wa awali ulibainika kuwa cheti cha mchezaji huyo kilionesha amezaliwa Colombia, Lakini ikaonekana aliingia Ecuador kinyemela kutafuta maisha, na baadae Shirikisho la Soka la Ecuador (FEF) likashiriki kumtengezea nyaraka za uongo ili kuthibitisha uraia wake.

 

FIFA Yaisamehe Chile na Peru

Na baadae kamati ya Rufaa (FIFA) ilikutana Septemba 15 2022 kujadili suala hilo la beki huyo aliyecheza mechi 8 za kuwania kufuzu Kombe la Dunia. Na ndipo FiFA wameamua kuyatupilia mbali mashitaka hayo hivyo mchezaji huyo ataendelea kuichezea Ecuador na watashiriki michuano hiyo ya Kombe la Dunia kama ilivyopangwa.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa