FIFA Kuiondoa Ecuador kwenye Mashindano ya Kombe la Dunia 2022

FIFA imemwita mchezaji wa kimataifa wa Ecuador Byron Castillo kusikiliza kesi yake siku ya Alhamisi jijini Zurich Uswisi ilikuthibitisha uhalali wake wa utaifa kutoka na mahojiano aliyoyafanya hivi karibuni.

Kwenye jumbe ya sauti uliyochapiswa na Sportsmail siku ya jumatatu, Castillo alitaja jina na tarehe ya kuzaliwa ambayo ilifanana na cheti chake cha kuzaliwa cha Colombia, ma alieleza kuwa alitoka Tumaco kwenda San Lorenzo, Ecuador ili kuapata nafasi ya kujiendeleza karia yake.

Pia Castilo alimteja mfanya biashara ambaye anadai alimpatia cheti kipya cha kuzaliwa. Sintofahamu hii aliyoitengeneza inaweza pelekea timu ya taifa ya Ecuadoor kuondolewa kwenye mashindano ya kombe la dunia mwaka huu na kupelekea timu ya taifa ya Chile kuchukua nafasi yake.

Ikiwa imebaki miezi miwili kabla ya kombe la dunia kuanza, Chile wanaweza kupata nafasi ikiwa  FIFA watawazasia ushindi kwenye michezo miwili ambayo Castilo alicheza dhidi yao, ingawa kuna uwezekano mwengine kati Peru au Italia wanaweza kupewa nafasi ya kushiriki michuano hiyo.

Rais wa shirikisho la soka chile leo, alisema kuwa kutoka kwenye kinywa cha mchezaji ametambua utaifa na kila kitu alichofanya hii itawapa nguvu na kutumia kama ushaidi ambao watauwasilisha.

Kesi ya awali Chile walishindwa kwa sababu ya kutokuwa na ushaidi wa kutosha ili kuweza kuwaondoa Ecaudor kwenye mashindano ya kombe la dunia kwa kumchezesha mchezaji wa taifa jingine.

Acha ujumbe