Carlos Queiroz amethibitisha kuwa kwenye mashindano ya kombe la dunia yanayayotarajiwa kufanyika kwenye majira ya baridi nchini Qatar atainoa timu ya taifa ya Iran.

Carlos Queiroz mwenye miaka 69, awali alikuwa akiinoa timu ya taifa ya misri. Carlos hii ni mara yake ya tatu kuinoa timu ya taifa ya iran kwenye michuano ya kombe la dunia, aliongoza taifa mwaka 2014 na 2018.

Carlos Queiroz, Carlos Queiroz Kuinoa Iran kwenye Michuano ya Kombe La Dunia 2022, Meridianbet

Kocha huyo wa zamani wa klabu ya Real Madrid anarejea kuinoa timu ya taifa ya Iran kukiwa kumebakia miezi miwili kabla ya kuanza kwa michuano ya kombe la dunia nchini Qatar.

Carlos Queiroz, pia alishawai kufanya kazi na Sir Alex Ferguson kama kocha msaidizi kwenye klabu ya Manchester United, alipochukua nafasi ya Dragan Skocic ambaye aliongoza Iran kwenye michezo ya kufuzu kwa upande wa Asia.

Iran ipo kundi B ambalo linatimu England, Wales na USA, na kikosi cha  Querioz  kinatarajiwa kucheza mchezo wa ufunguzi wa kundi B dhidi ya England jumatatu November 21.

“Familia inapokwita nyumbani, unachopaswa kufanya ni kujionyesha. Kujizatiti kwenye majukumu yako na kuwa tayari kwa misheni. Tufanye hili kwa pamoja! kwa ajiri ya kesho! Asanteni sana Timu Melli.”

Aliandika Queiroz

Iran, kwenye michuano ya kombe la dunia wanashiriki kwa mara ya sita tokea kuanzishwa kwake, pia wanataraji mwaka huu kuvunja rekodi ya kuishia hatua ya makundi na kuendelea kwenye hatua ya 16 bora.

 

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa