WAKITARAJIA kumenyana na Kitayosce, Uongozi wa Pan African umefunguka kuwa malengo yao kwa msimu huu ni kuhakikisha wanapata nafasi ya kupanda ligi kuu.

Pan Yapania Kupanda Ligi Kuu

Klabu hiyo ambayo inashiriki michuano ya Championship kwa msimu huu inatarajia kucheza mchezo wake wa kwanza kwenye ligi dhidi ya Kitayosce ya Tabora, Septemba 17, mwaka huu.

Akizungumzia malengo yao, Ofisa Habari wa Klabu hiyo yenye makao makuu yake Jijini Dar Es Salaam, Leen Essau alisema kuwa “Kikosi chetu kinaendelea vizuri na maandalizi ya mchezo wetu wa kwanza dhidi ya Kitayosce.

Pan Yapania Kupanda Ligi Kuu

“Timu tayari imeondoka Dar kwa ajili ya mchezo huo na mipango yetu ni kupata pointi sita katika michezo miwili ya ugenini ambayo tutaenda kucheza dhidi ya Kitayosce na Mashujaa.

“Malengo tuliyojiwekea kwa msimu huu ni kuhakikisha haturudii makosa ambayo tumeyafanya kwa msimu uliopita na kutafuta nafasi ya kushiriki ligi kuu kwa msimu ujao.”

Pan Yapania Kupanda Ligi Kuu

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa