Klabu ya Pan African inatarajia kufanya uchaguzi wa viongozi mbalimbali Agosti 13 mwaka huu kwenye ukumbi wa maafisa wa Polisi Oysterbay jijini Dar es Salaam.

Akizungumzia uchaguzi huo, Ofisa Habari wa Pan African, Leen Essau amesema kuwa Viongozi ambao watachaguliwa ni Mwenyekiti, Makamu mwenyekiti na wajumbe sita.

Pan
Pan African

Fomu zinapatikana makao makuu ya klabu yaliyopo mtaa wa Swahili na Kariakoo, ambapo gharama za Fomu kwa nafasi ya Mwenyekiti ni laki mbili (200,000), Makamu Mwenyekiti ni laki mbili (200,000) na Wajumbe ni laki moja (100,000) kwa kila mgombea.

Fomu hizo zitaanza kutolewa Julai 25 mwaka huu na mwisho wa kurudisha ni Julai 30. Uongozi unawaomba wanachama kuchukua fomu mapema ili kumaliza zoezi hili kwa wakati uliopangwa.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa