Klabu ya Barcelona imeingia kwenye mbio za kuhitaji huduma ya mlinzi wa kimataifa kutoka Ufaransa anayekipiga kwenye klabu ya Sevilla Jules Kounde.

Klabu ya Chelsea imeanda kitita cha €65milioni ili kuweza kuhakikisha wanapata huduma ya mlinzi wa kimataifa kutoka Ufaransa na hadi sasa washafanya makubaliano binafsi na mchezaji huyo.

Barcelona, Barcelona Kuiharibia Chelsea, Meridianbet

Chelsea kwa sasa uhamisho wa Kounde hautakuwa mwepesi tena baada ya klabu ya Barca kuingilia kati kutaka huduma ya mlinzi huyo awali The blues walishindwa kufanikisha usajiri wa kiungo wa kimatifa kutoka brazili Raphinha baada ya barcelona kuihataji hudumaya kiungo huyo.

Jules Kounde ameachwa kwenye kikosi cha sevilla ambacho kimeweka kambi nchini Ureno kwa ajiri ya maandilizi ya michezo ya msimu huu inayotarajiawa kuanza kmwezi August.

Barcelona wanajua kuwa hawawezi kushindana na Chelsea kifedha kwaiyo wanajitahidi kumshawishi mchezaji huyo ili wapate unafuu kwenye uhamisho huo.

Mpaka sasa Barcelona hajapeleka offer yoyote rasmi kwa klabu ya Sevilla

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa