BAADA ya kupoteza mchezo wa kwanza dhidi ya Hilal Al Sahil kwa bao 1-0, hatimaye Geita Gold wamerejea Dar kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa marudiano.

Geita Gold Yarejea Kibabe

Kikosi hicho kesho jumatano kitacheza mchezo wa ligi kuu dhidi ya Singida Big Stars huku jumamosi ikitarajia kucheza mechi ya marudiano dhidi ya Hilal Al Sahil ya Sudan.

Geita Gold Yarejea Kibabe

Mchezo huo wa marudiano utapigwa kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar ambapo ili Geita waweze kuvuka hatua hiyo wanapaswa kushinda mabao 2-0.

Geita Gold Yarejea Kibabe

Akizungumzia hilo, Ofisa Habari wa Klabu hiyo, Hemed Kivuyo amesema kuwa “Kikosi tayari kimerejea Dar kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa ligi dhidi ya Singida Big Stars.

“Wachezaji ambao hawakwenda na timu nchini Sudan tayari wameungana na wenzao kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa marudiano dhidi ya Hilal Al Sahil.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa