Klabu ya West Ham United wameonesha nia kumuhitaji beki wa kimataifa wa Uingereza anaekipiga klabu ya Manchester United Harry Maguire ambapo klabu hiyo imemueka sokoni.
West Ham chini ya kocha David Moyes wanataka kuboresha kikosi chao kwenye safu ya ulinzi ambapo wanamuona Maguire kama mtu sahihi, Lakini kikwazo ni dau ambalo Man United wanahitaji kwajili ya kumuuza beki huyo.
Man United wanahitaji kiasi cha paundi milioni 50 kwa klabu ambayo itahitaji huduma ya Harry Maguire, Hivo kinachosubiriwa ni klabu hiyo kutoka jijini London kutuma ofa rasmi kwa masheteni hao wekundu kwajili ya beki huyo.
Taarifa za ndani kutoka kwa watu wa karibu wa beki huyo zinaeleza kua Maguire amewekwa sokoni, Lakini yeye mwenyewe anataka kuendelea kubaki ndani ya klabu ya Man United kwani anaona anaweza kupambania nafasi kitu ambacho kinaweza kuweka ugumu kwa West Ham kunasa saini ya beki huyo.
Maguire mpaka sasa sio chaguo la mwalimu Ten Hag kwenye kikosi cha Manchester United, Hivo ni wazi atakua na mazingira magumu akibakia ndani ya timu hiyo kuelekea msimu ujao na hapo West Ham wanaona ni kama nafasi kwao ya kumpata beki huyo.

