Kocha wa klabu ya Barcelona Xavi Hernandez amesema mshambuliaji kijana ndani ya klabu hiyo Ansu Fati hawezi kujiunga na mahasimu wao klabu ya Real Madrid.
Kocha Xavi amesisitiza kua mchezaji Ansu Fati bado ataendelea kua mchezaji muhimu ndani ya klabu hiyo, Hivo taarifa za yeye kujiunga na klabu ya Real Madrid sio za kweli na ni jambo ambalo haliwezekani.
Kocha huyo anasema Ansu Fati ni kama nembo au urithi wa klabu hiyo kwahiyo sio jambo jepesi kwa yeye kuondoka ndani ya klabu hiyo, Lakini pia hiyo ni kutokana na kijana huyo kuibuliwa kutoka kwenye akademi ya klabu hiyo.
Kuna taarifa mbalimbali ambazo zimekua zikimhusisha Ansu Fati kuondoka ndani ya klabu ya Barcelona, Hii ikiwa inatokana na mchezaji huyo kukosa nafasi ya kudumu ndani ya klabu hiyo tofauti na matarajio ya wengi yalivyokua.
Mshambuliaji Ansu Fati ambaye ni zao la klabu ya Barcelona La Masia amekua akiandamwa na majeraha ya mara kwa mara ikiwa ni moja ya sababu ambayo inaelezwa kuwafanya Barcelona kufikiria kumuuza, Lakini Kocha Xavi yeye amekataa kuhusiana na jambo la mshambuliaji huyo kuuzwa haswa kwenda Real Madrid.

