Nahodha wa Italia, Gianluigi Donnarumma, yupo mbioni kujiunga na Manchester City kwa ada ya uhamisho ya €27 milioni na mshahara wa awali wa €15 milioni.

Kwa mujibu wa taarifa za Football Italia, Manchester City wamefikia makubaliano ya kumsajili Donnarumma kutoka PSG kwa takribani €27 milioni.
Mkataba wa kimataifa huyo wa Italia na PSG unatarajiwa kumalizika Juni 2026, na sasa mabingwa hao wa Premier League wamekamilisha makubaliano ya kuhakikisha sahihi yake.
Vyanzo vya kuaminika vimedokeza kuwa Donnarumma atasaini mkataba wa miaka mitano ukiwa na kipengele cha kuongeza mwaka mmoja zaidi.
Atalipwa €15 milioni katika mwaka wa kwanza, kisha €16 milioni kwa mwaka wa pili na wa tatu, na €17 milioni kwa miaka miwili ya mwisho ya mkataba wake na City.


