Donnarumma Kukamilisha Uhamisho wa Pauni Milioni 27 kwenda Manchester City

Nahodha wa Italia, Gianluigi Donnarumma, yupo mbioni kujiunga na Manchester City kwa ada ya uhamisho ya €27 milioni na mshahara wa awali wa €15 milioni.

Donnarumma Kukamilisha Uhamisho wa Pauni Milioni 27 kwenda Manchester City

Kwa mujibu wa taarifa za Football Italia, Manchester City wamefikia makubaliano ya kumsajili Donnarumma kutoka PSG kwa takribani €27 milioni.

Mkataba wa kimataifa huyo wa Italia na PSG unatarajiwa kumalizika Juni 2026, na sasa mabingwa hao wa Premier League wamekamilisha makubaliano ya kuhakikisha sahihi yake.

Vyanzo vya kuaminika vimedokeza kuwa Donnarumma atasaini mkataba wa miaka mitano ukiwa na kipengele cha kuongeza mwaka mmoja zaidi.

Atalipwa €15 milioni katika mwaka wa kwanza, kisha €16 milioni kwa mwaka wa pili na wa tatu, na €17 milioni kwa miaka miwili ya mwisho ya mkataba wake na City.

Donnarumma Kukamilisha Uhamisho wa Pauni Milioni 27 kwenda Manchester City

Donnarumma tayari amewaaga mashabiki wa PSG baada ya mechi yao ya kwanza ya nyumbani tarehe 22 Agosti. Nyota huyo wa Italia alijiunga na PSG bila malipo akitokea AC Milan majira ya kiangazi ya mwaka 2021.

Kipa huyo ameitumikia PSG kwenye michezo 161, akifanikiwa kutwaa mataji manne ya Ligue 1 pamoja na ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu wa 2024-25.

Kwa sasa, Donnarumma ameitwa na kocha mpya wa Italia, Gennaro Gattuso, kwa ajili ya michezo ya kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Estonia na Israel mwezi huu.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.