Mkurugenzi wa Como, Carlalberto Ludi, amethibitisha kuwa Cesc Fabregas alikuwa mchezaji wa kiwango cha dunia na ni bora zaidi kama kocha akifanya kazi na klabu yenye malengo yasiyo na mipaka.

“Dhamira yetu ni kuendelea kukua, wiki baada ya wiki, kupitia kazi ya Cesc na kikosi mazoezini,” alisema Ludi akizungumza na Sport Mediaset.
Mkurugenzi huyo amesema kuwa hawawezi kujua watafika wapi, lakini malengo ya klabu hiyo hayana mipaka. Wanataka kuendelea kupandisha kiwango kila wakati.
Daima ni tukio maalum Fabregas anapokutana na Antonio Conte, ambaye aliwahi kuwa kocha wake wakati Chelsea iliposhinda Kombe la FA.
Tayari walishakutana mapema msimu huu katika sare ya 0-0 kwenye Uwanja wa Maradona katika Serie A, ambapo Vanja Milinkovic-Savic aliokoa penalti ya Alvaro Morata.
Vilabu vikubwa vinaaminika kuwa vinamfuatilia kocha huyo, hivyo je Como wana wasiwasi kuhusu uwezekano wa Fabregas kupewa ofa?


