PSG Yalipa Kisasi, Yaichapa 5-2 Chelsea UCL

Klabu ya PSG imejiweka katika nafasi nzuri ya kusonga mbele hatua ya robo fainali ya UEFA Champions League baada ya kuifunga Chelsea FC mabao 5-2 katika mchezo wa kwanza wa hatua ya 16 bora uliochezwa kwenye Uwanja wa Parc des Princes. Ushindi huo unaipa PSG faida ya mabao matatu kabla ya mchezo wa marudiano utakaochezwa jijini London wiki ijayo.

PSG Yalipa Kisasi, Yaichapa 5-2 Chelsea UCL

PSG ilianza mchezo huo kwa kasi kubwa ikilenga kulipiza kisasi cha kipigo walichopata kwenye fainali ya Kombe la Dunia la Klabu mwaka uliopita. Bao la kwanza lilipatikana baada ya kichwa cha João Neves kumkuta Bradley Barcola ambaye alipiga shuti kali lililogonga mwamba wa juu wa lango na kuingia wavuni.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Baada ya bao hilo, Chelsea FC walijibu mashambulizi na kufanikiwa kusawazisha kupitia Malo Gusto aliyefunga baada ya kupokea pasi ndefu kutoka kwa Enzo Fernández. Hata hivyo, kabla ya mapumziko Ousmane Dembélé alifunga bao la pili kwa PSG akimalizia shambulizi la kushtukiza na kurejesha uongozi kwa wenyeji.

Hata hivyo, makosa ya kipa Filip Jørgensen yaliigharimu Chelsea baada ya kiungo Vitinha kufunga bao la tatu la PSG kufuatia pasi ya Khvicha Kvaratskhelia. Chelsea walidhani wamesawazisha kupitia João Pedro lakini bao hilo lilikataliwa kwa kuotea.

PSG Yalipa Kisasi, Yaichapa 5-2 Chelsea UCL

PSG waliendelea kushambulia hadi dakika za mwisho ambapo Kvaratskhelia alifunga bao la nne kwa shuti kali lililokwenda kona ya mbali ya lango. Dakika za nyongeza, mshambuliaji huyo wa Georgia aliongeza bao la tano baada ya kumalizia krosi ya Achraf Hakimi. Akizungumzia ushindi huo, kocha wa PSG Luis Enrique alisema, “Tulicheza kwa nguvu kubwa na kuonyesha ubora wetu, lakini bado tunapaswa kubaki makini kwa sababu mchezo wa marudiano utakuwa na ushindani mkubwa.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.