Beki wa Yanga SC na nahodha msaidizi wa timu hiyo, Dickson Job, ametoa ujumbe wa shukrani kwa ndugu, jamaa, marafiki na mashabiki wa klabu hiyo kufuatia sapoti kubwa aliyopata baada ya kufanyiwa upasuaji hivi karibuni nchini Afrika kusini. Mchezaji huyo amesema ameguswa sana na upendo aliouonyeshwa katika kipindi cha changamoto ya kiafya anachopitia.

Job alieleza kuwa ujumbe wa faraja, maombi na maneno ya kutia moyo aliyopokea kutoka kwa watu mbalimbali umempa nguvu na matumaini makubwa ya kuendelea na matibabu yake huku akijiandaa kurejea uwanjani siku zijazo.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Nyota huyo wa Yanga alisema sapoti kutoka kwa viongozi wa klabu, wachezaji wenzake pamoja na mashabiki imeonyesha kwa namna gani familia ya Wananchi ina mshikamano mkubwa wakati wa changamoto.
“Kwa moyo wa shukrani napenda kuwashukuru sana ndugu, jamaa na marafiki wote kwa salamu zenu za pole, maombi na faraja mlizonipa baada ya kufanyiwa upasuaji,” alisema Job katika ujumbe wake wa shukrani.

