Viongozi wa Simba SC Wamtembelea Wilson Nangu

Viongozi wa klabu ya Simba SC wamemtembelea beki wao Wilson Nangu nyumbani kwao Boma Ng’ombe, mkoani Kilimanjaro ili kumjulia hali wakati akiendelea kupona majeraha. Ziara hiyo imefanyika leo Machi 13, 2026 ikiwa ni sehemu ya kuonyesha mshikamano na sapoti kwa mchezaji huyo.

Viongozi wa Simba SC Wamtembelea Wilson NanguUongozi huo uliongozwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa klabu hiyo, Crescentius Magori ambaye aliambatana na Mjumbe wa Bodi Swedi Mkwabi, Mjumbe wa Kamati ya Mashindano Habibu Nasser pamoja na Meneja wa Habari na Mawasiliano wa klabu hiyo Ahmed Ally.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Lengo la ziara hiyo lilikuwa kumtia moyo mchezaji huyo pamoja na kufuatilia maendeleo ya afya yake baada ya kufanyiwa upasuaji kufuatia jeraha alilolipata hivi karibuni. Viongozi hao pia walipata nafasi ya kuzungumza naye pamoja na familia yake kuhusu hatua ya matibabu anayoendelea nayo.

Viongozi wa Simba SC Wamtembelea Wilson NanguBeki huyo alipata jeraha la kifundo cha mguu katika mchezo wa CAF Champions League wakati Simba ilipokutana na Espérance Sportive de Tunis. Baada ya tukio hilo alipelekwa kwa matibabu zaidi ambapo alifanyiwa upasuaji nchini South Africa.

Viongozi wa Simba SC Wamtembelea Wilson NanguKwa sasa, Nangu anaendelea na hatua ya kupona nyumbani huku akipata uangalizi wa kitabibu, na klabu imeeleza matumaini yake kuwa mchezaji huyo atarejea uwanjani baada ya kukamilisha ipasavyo programu ya matibabu na mazoezi ya kurejea katika hali ya kawaida.

 

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.