Bayern Wameweka Wazi Msimamo Wao Kuhusu Uwezekano wa Michael Olise Kuhamia Liverpool

Afisa wa FC Bayern Munich, Uli Hoeness, ameiambia Liverpool  kuwa vigogo hao wa Ujerumani hawatakuwa sehemu ya kusaidia mipango yao ya usajili, huku pia akitoa kijembe kuhusu msimu wao usioridhisha licha ya kutumia fedha nyingi majira ya joto.

Bayern Wameweka Wazi Msimamo Wao Kuhusu Uwezekano wa Michael Olise Kuhamia Liverpool

Liverpool wamepata pigo kubwa kufuatia tangazo la kushtukiza kwamba Mohamed Salah ataondoka klabuni mwishoni mwa msimu wa 2025-26, jambo linalomaanisha kuwa watalazimika kutafuta mbadala wake.

Mohamed Salah amekubali kuvunja mkataba wake mapema, hatua inayoiwezesha Liverpool kuondokana na majukumu ya mishahara ya baadaye.

Nyota wa FC Bayern Munich, Michael Olise, amekuwa kwenye orodha ya matamanio ya Liverpool kwa muda sasa, na kuondoka kwa Salah kunaweza kuisukuma klabu hiyo kufanya jitihada kubwa za kumsajili majira haya ya joto.

Hata hivyo, FC Bayern Munich hawana kabisa nia ya kumuachia winga huyo Mfaransa Michael Olise kuondoka, na pia hawana hamu yoyote ya kufanya biashara na Liverpool.

Bayern Wameweka Wazi Msimamo Wao Kuhusu Uwezekano wa Michael Olise Kuhamia Liverpool

Uli Hoeness ni nembo halisi ya FC Bayern Munich, akitumia misimu tisa klabuni hapo kama mchezaji kabla ya kuingia kwenye nafasi za uongozi. Kwa sasa, mwenye umri wa miaka 74 ni mjumbe wa bodi, baada ya pia kuwahi kuwa rais wa klabu na meneja mkuu.

Katika mahojiano ya hivi karibuni na DPA, Hoeness aliweka wazi kabisa msimamo wake iwapo Liverpool watajaribu kumsajili Michael Olise kwenda Merseyside.

“Mkumbuke Liverpool walitumia €500 milioni majira ya joto yaliyopita na bado wana msimu mbaya sana. Hivyo hatutachangia wao kucheza vizuri zaidi msimu ujao.” Alisema.

FC Bayern Munich wanaendelea kufanya vizuri katika Bundesliga na wamefuzu hatua ya robo fainali ya UEFA Champions League, huku Michael Olise akiwa mhimili mkubwa wa mafanikio hayo.

Winga huyo Mfaransa amefunga mabao 11 na kutoa pasi za mabao 18 katika mechi 25 za Bundesliga, pamoja na kuongeza mabao matatu na pasi nne za mabao katika mechi tisa za Champions League.

Bayern Wameweka Wazi Msimamo Wao Kuhusu Uwezekano wa Michael Olise Kuhamia Liverpool

Bayern walimsajili Olise kutoka Crystal Palace mwaka 2024, na sasa wanamuona kama mmoja wa vipaji bora zaidi duniani. Ana mkataba hadi 2029 na inaripotiwa kuwa hana kipengele cha kuachiliwa (release clause).

Ingawa amekuwa akivutia klabu kubwa kama Real Madrid CF na Liverpool, Bayern wanasisitiza kuwa hauzwi. Mkurugenzi wa michezo wa Bayern, Max Eberl, pia alipuuza kabisa uwezekano wa Olise kuondoka katika mazungumzo na Sport Bild

“Hatuwazii hata kidogo hilo. Yeye ni mchezaji wa Bayern Munich na ana kila fursa hapa ambayo wachezaji wakubwa wanahitaji. Tunataka kujenga mustakabali pamoja naye.”

Afisa mkuu mtendaji wa klabu hiyo, Jan-Christian Dreesen, alisisitiza msimamo huo huo akisema: “Haijalishi ni klabu gani itajaribu kumshawishi: yeyote anayeichezea Bayern Munich anajua thamani ya kuwa hapa.”

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.