Kompany Asema Bayern Ilistahili Ushindi Baada ya Kupambana Kiakili na Real madrid

Kocha wa Bayern Munich, Vincent Kompany, amewapongeza wachezaji wake kufuatia ushindi wa kusisimua dhidi ya Real Madrid katika mchezo wa mkondo wa pili wa robo fainali ya UEFA Champions League uliopigwa kwenye Uwanja wa Allianz Arena.

Kompany Asema Bayern Ilistahili Ushindi Baada ya Kupambana Kiakili na Real madridBayern iliibuka na ushindi wa mabao 4-3, ikiwa ni matokeo yaliyopatikana kwa jitihada kubwa, hasa kupitia mabao ya dakika za mwisho yaliyofungwa na Luis Diaz na Michael Olise, ambayo yaliamua hatima ya mchezo huo wenye ushindani mkubwa.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Akizungumza baada ya mchezo, Kompany alisema ulikuwa mchezo wenye hisia kali na changamoto nyingi kwa pande zote mbili, akisisitiza kuwa Real Madrid walionesha ubora wao wa kawaida katika michuano ya Ulaya.

Kompany Asema Bayern Ilistahili Ushindi Baada ya Kupambana Kiakili na Real madrid“Ulikuwa mchezo wa hisia sana. Tulipata nafasi nyingi na kila mara tulihisi tunaweza kufunga, lakini Real Madrid inabaki kuwa Real Madrid,” alisema Kompany.

Aliongeza kuwa wachezaji wake walionesha uimara wa kiakili licha ya presha kubwa ya mchezo, huku akiwapongeza pia mashabiki kwa sapoti yao kubwa uwanjani Allianz Arena ambayo iliwapa nguvu zaidi.

Kompany Asema Bayern Ilistahili Ushindi Baada ya Kupambana Kiakili na Real madrid“Wachezaji wangu walikuwa imara kiakili leo, na mashabiki pia walitusaidia sana. Tulitulia na kila mara tulihisi wakati wetu ungefika. Vijana walistahili ushindi huu,” alimalizia Kompany.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.