Kocha wa Arsenal FC, Mikel Arteta, ameweka rekodi ya kihistoria baada ya kuwa kocha wa kwanza katika klabu hiyo kuifikisha timu hiyo hatua ya nusu fainali ya UEFA Champions League kwa misimu miwili mfululizo.
Arsenal ilitinga hatua hiyo baada ya sare ya bila kufungana 0-0 dhidi ya Sporting CP, matokeo yaliyowapa ushindi wa jumla wa 1-0 na kuendeleza safari yao ya kuisaka taji la kwanza la michuano hiyo mikubwa barani Ulaya.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Akizungumza baada ya mchezo, Arteta aliwaomba mashabiki wa Arsenal kuthamini mafanikio hayo makubwa badala ya kuendelea kukosoa kiwango cha uchezaji wa timu hiyo, akisisitiza kuwa wanachokifanya ni cha kipekee na cha kihistoria.
“Haijawahi kufanyika kwa miaka 140,” alisema Arteta. “Furahieni pale tulipo. Hii si jambo la kawaida, ni hatua kubwa sana kwa klabu hii.” Aliongeza kuwa licha ya mafanikio hayo, timu bado ina maeneo ya kuboresha, lakini alisisitiza kuwa mafanikio waliyoyapata yanapaswa kupewa heshima kubwa na kuthaminiwa na mashabiki na wadau wa soka.
“Sisi si wakamilifu,” alisema. “Lakini tumefanya kazi kubwa sana kufika hapa tulipo, na bado tunaendelea kujifunza na kuboresha kila siku.”
Arsenal sasa inajiandaa kwa mtihani mgumu wa nusu fainali dhidi ya Atletico Madrid, ambapo itaanzia ugenini katika mchezo wa mkondo wa kwanza utakaopigwa Aprili 29, 2026 katika Uwanja wa Riyadh Air Metropolitano.
Mchezo wa marudiano utachezwa Emirates Stadium Mei 5, 2026, na mshindi wa jumla ya mikondo hiyo miwili ndiye atakayetinga fainali ya UEFA Champions League msimu huu.

