Klabu ya Al Ahli imefanikiwa kutinga fainali ya AFC Champions League Elite baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Vissel Kobe katika mchezo wa nusu fainali uliochezwa jijini Jeddah.
Mabingwa watetezi walijikuta nyuma mapema baada ya Yoshinori Muto kuifungia Vissel Kobe bao la kuongoza dakika ya 31, kufuatia mpira wa adhabu uliopigwa na Katsuya Nagato na kupanguliwa vizuri na Yuya Osako kabla ya kumkuta Muto aliyefunga kwa urahisi.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Al Ahli walirejea kwa nguvu kipindi cha pili, ambapo Galeno alisawazisha dakika ya 62 kwa shuti kali lililomshinda kipa Daiya Maekawa. Shinikizo lao liliendelea kuongezeka, huku wakikaribia kufunga mara kadhaa kupitia Ivan Toney na Franck Kessié.
Dakika ya 70, Toney alihakikisha ushindi kwa kufunga bao la pili baada ya kutumia vyema krosi ya Galeno, akipenya katikati ya mabeki wa Kobe na kuipeleka timu yake mbele kwa ustadi mkubwa.
Akizungumza baada ya mchezo, kocha wa Al Ahli Matthias Jaissle alisema, “Tunajivunia kufika fainali tena mfululizo. Hili ni jambo maalum na heshima kubwa kwetu. Mechi ilikuwa ngumu na maamuzi madogo ndiyo yaliyoamua matokeo.”
Kwa ushindi huo, Al Ahli sasa wanasubiri mshindi kati ya Shabab Al Ahli na Machida Zelvia ili kukamilisha fainali, huku wakilenga kuwa timu ya kwanza tangu Al Ittihad mwaka 2005 kutwaa taji hilo mara mbili mfululizo.

