Arsène Wenger Aamini Arsenal FC Bado Wana Nafasi Kubwa ya Ubingwa EPL

Kocha wa zamani wa Arsenal, Arsène Wenger, ameibuka na kauli yenye uzito mkubwa kuhusu mbio za ubingwa wa EPL msimu wa 2025/26, akisisitiza kuwa Arsenal bado wana nafasi kubwa ya kunyakuwa taji hilo licha ya kupoteza mchezo muhimu dhidi ya Manchester City hivi karibuni.

Arsène Wenger Aamini Arsenal FC Bado Wana Nafasi Kubwa ya Ubingwa EPLWenger ameonyesha imani kubwa kwa timu hiyo aliyowahi kuinoa kwa mafanikio makubwa.“Naamini Arsenal itashinda ligi… Manchester City hawatakuwa na mwisho mzuri wa msimu,” amesema Wenger, akitoa mtazamo wake juu ya ushindani mkali uliopo kileleni mwa msimamo wa ligi. Kauli hiyo imekuja wakati ambapo Arsenal wanaongoza msimamo kwa tofauti ndogo ya pointi, jambo linaloonyesha kuwa mbio za ubingwa bado ziko wazi kabisa.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Kwa sasa, Arsenal wamecheza mechi 33 na kukusanya pointi 70, wakiongoza jedwali, huku Manchester City wakiwa na pointi 67 baada ya kucheza mechi 32. Hii ina maana kuwa City wana faida ya mechi moja mkononi, ambayo inaweza kuwafanya kufikia au hata kupita Arsenal iwapo watashinda mchezo huo wa kiporo dhidi ya Crystal Palace FC.

Arsène Wenger Aamini Arsenal FC Bado Wana Nafasi Kubwa ya Ubingwa EPLRatiba ya mechi zilizobaki kwa Arsenal inaonekana kuwa na mchanganyiko wa changamoto na fursa, ambapo wanatarajiwa kuikaribisha Newcastle United FC Aprili 25, kabla ya kukutana na Fulham FC Mei 2, zote nyumbani. Baadaye watasafiri kucheza dhidi ya West Ham United kabla ya kumalizia msimu kwa michezo dhidi ya Burnley FC na Crystal Palace.

Kwa upande wa Manchester City, ratiba yao inaonekana kuwa ndefu zaidi kutokana na mchezo wa kiporo. Wanatarajiwa kukutana na Burnley, Everton FC, Brentford FC, AFC Bournemouth, Aston Villa pamoja na Crystal Palace. Ratiba hii inaweza kuwa na athari kubwa katika mbio za ubingwa kutokana na idadi ya mechi na ushindani wake.

Arsène Wenger Aamini Arsenal FC Bado Wana Nafasi Kubwa ya Ubingwa EPLKwa ujumla, kauli ya Wenger imeongeza moto katika mbio za ubingwa huku mashabiki wakisubiri kuona kama Arsenal watahimili presha ya mwisho wa msimu au kama Manchester City watatumia faida ya mechi yao ya ziada kubadilisha mwelekeo wa taji. Mbio hizi zinaendelea kuwa za kusisimua huku kila pointi ikiwa na uzito mkubwa katika kuamua bingwa wa msimu huu.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.