Klabu ya Feyenoord Rotterdam inaripotiwa kumuweka kwenye rada yake Giovanni van Bronckhorst katika harakati za kupata mkurugenzi mpya wa ufundi.
Kwa mujibu wa taarifa mbalimbali, Feyenoord bado hawajawasiliana rasmi na Liverpool F.C., ambako Van Bronckhorst kwa sasa ni sehemu ya benchi la ufundi, lakini inaelezwa kuwa yuko tayari kusikiliza ofa kutoka kwa klabu hiyo aliyowahi kuitumikia kwa mafanikio.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Van Bronckhorst aliichezea Feyenoord mechi 249 na baadaye kuiongoza kama kocha, akishinda mataji matano ikiwemo ubingwa wa ligi ya Uholanzi mwaka 2017, uliokuwa wa kwanza kwa klabu hiyo ndani ya miaka 18.
Katika taarifa, imeelezwa, “Feyenoord wanaona uzoefu na historia ya Van Bronckhorst ndani ya klabu hiyo kuwa ni nyenzo muhimu kwa nafasi ya mkurugenzi wa ufundi.”
Nafasi hiyo imeachwa wazi baada ya Dennis te Kloese kutangaza kuondoka, huku akiwahi pia kushika majukumu hayo tangu mwaka 2022 baada ya kuondoka kwa Frank Arnesen.
Kabla ya kujiunga na Liverpool mwaka 2025 kama msaidizi wa Arne Slot, Van Bronckhorst aliwahi kufundisha klabu mbalimbali zikiwemo Rangers F.C. na kufika fainali ya UEFA Europa League mwaka 2022.

