Unai Emery Ataka Kuandika Historia Mpya Ulaya Europa League

Kocha wa Aston Villa, Unai Emery, amesema anataka kuandika “ukurasa mpya” wa mafanikio barani Ulaya wakati kikosi chake kikijiandaa kukutana na Nottingham Forest katika nusu fainali ya UEFA Europa League.

Unai Emery Ataka Kuandika Historia Mpya Ulaya Europa LeagueTimu hizo mbili za Ligi Kuu England zitakutana katika mchezo wa mkondo wa kwanza Alhamisi kwenye uwanja wa City Ground, zikiwa hatua moja tu kufuzu fainali ya mashindano ya Ulaya kwa mara ya kwanza baada ya miongo kadhaa. Forest waliwahi kushinda Kombe la Ulaya mwaka 1979 na 1980, huku Villa wakitwaa taji hilo mwaka 1982.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Emery, ambaye ameibadili Villa tangu alipochukua mikoba mwaka 2022, bado hajafanikiwa kuipa timu hiyo taji kubwa ndani ya miaka 30. Msimu wa 2023/24 walitolewa nusu fainali ya UEFA Europa Conference League na Olympiakos, kabla ya kupoteza tena nusu fainali ya FA Cup dhidi ya Crystal Palace.

Unai Emery Ataka Kuandika Historia Mpya Ulaya Europa LeagueAkizungumza kabla ya mchezo huo, Emery alisema “Tunataka kutumia uzoefu wetu kuboresha kiwango chetu, lakini tunafahamu kuwa nusu fainali ni ngumu sana kwa sababu nafasi ni 50 kwa 50 kati ya timu zote mbili.”

Unai Emery Ataka Kuandika Historia Mpya Ulaya Europa LeagueAliongeza kuwa “Wana wachezaji wazuri, kocha mwenye uzoefu Ulaya, na wako kwenye kiwango kizuri kwa sasa, jambo linalowapa kujiamini zaidi.”

Unai Emery Ataka Kuandika Historia Mpya Ulaya Europa LeagueLicha ya mafanikio yake makubwa kwenye Europa League akiwa na Sevilla na Villarreal, Emery alisisitiza kuwa anaanza ukurasa mpya, akisema “Kila kilichopita kimekwisha, sasa ni mwanzo mpya na nataka kuandika historia mpya hapa.”

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.