kazitazame tena pasi za mjerumani. Mesut Ozil. Nasema hivi, leo achana na wote, kaitazame tena miguu ya Mturuki. Mesut Ozil. Mtoto fulani kutoka Ujerumani Magharibi. Mwezi mmoja tu baada ya kusheherekea birthday yake ya kwanza. Ukuta wa Berlin ulidondoka. Alikuja na Ujerumani mpya.

Ukawaulize maajabu yake pale Shalke 04 na Werder Bremen. Mimi nitakueleza kuanzia Real Madrid. Usiku ule wa December 11, Messi anavuja jasho pale Camp Nou, anawapiga chenga mabeki wanne na kunyanyua watu jukwaani. Ozil yeye aliwaacha watu wanne akiwa amesimama, pasi yake moja tu miguuni kwa Higuan, iliupita ukuta mzima wa Barca, walibaki wamesimama wanaangalia mpira unapitia hawajui wauzuie vipi.
Ile ndiyo tafsiri ya “playmaker”. Japo mara kadhaa ametumika kama winga, yeye anafurahi zaidi kutumika kama kiungo mchezeshaji. Jim Beglin wa skysports 2010 alisema Ozil amekuja na mpira mpya, Ujerumani walimtumia kama “false winger”, anachukua mpira kutoka kati kukimbilia pembeni. Ile haikuwahi kufanyika duniani.

Ozil ni ndoto ya kila Striker. Jiulize kwanini Rooney alikuwa anamshinikiza babu amsajili. Mourinho aliwahi kusema “Ozil ni wa tofauti sana, hakuna copy yake, hata copy yake mbaya haipo” Jiulize tena, kwanini Ronaldo alikasirika kipindi Ozil anaondoka. Assist 26 kwenye msimu wake wa mwisho na Madrid, 20 zote alizigonga kwa Ronaldo. Hata kama ni mimi nisingeacha mbachao.
Ule mguu wake wa kushoto, umeungana na sehemu ya macho yake. Kwenye ukuta ambao unadhani unapitika kwa chenga, yeye anaweza kuuacha kwa pasi moja tu. Mtakapoziba njia ardhini, yeye atamtafuta Striker wake hewani. Akizubaa anafunga yeye japo hapendi sana. Waulize wabelgiji kwenye EURO 2012 pale Poland & Ukraine .


John mwakalosi
Tuleteeni marlezo na makala zaid
Hidaya Mohamed
Asante meridianbet kwa taarifa
Frank patrick
SuperModifield…
Abram
⚽Mesut Ozil daaah huyuu jamaa ni bongee la mchezaji, ni winga mzuri na sio mchoyo Pasi za mwisho..
Sylvester
Huyu ni fundi wa pasi ila timu aliyeko sasa inamwangusha….safi sana meridianbet
Amani macha
Ni mchezaji asiyekuwa na makuu na mpira ana ujua vyema
Samira
Ozil ni kiungo mzuri sana katika uchezaji wake na anakila sifa ya kusajiliwa klabu kubwa zaidi arsenal
felister
Ozil ndo amenifanya mpk naipenda timu ya arsenal
Tahiya
Uyo jamaa namkubali kichizi natamani nangekuwepo kipindi kile cha kina henry enzi za arsenal kwnye ubora wao .
Ester jackson
Luiz ni mchezaji mzuri ila timu aliyo kuwepo ni mbaya
Furahav
Huyu jamaa namkubali sana.
aisha
Pongezi kwake