Msimamo wa UEFA Unakinzana na Ule wa FIFA

Mwenyekiti wa kamati ya matibabu wa UEFA anasema michuano inaweza kuanza tena licha ya mwenzake wa FIFA kusema haipaswi kuanza kabla ya Septemba. Mwenyekiti wa kitengo cha Matibabu cha Shirikisho la Soka barani Ulaya (UEFA) Tim Meyer amesema ni jambo linalowezekana kupanga mpango wa kuanza tena ligi za soka barani humo ili kumaliza sehemu ya msimu iliyobakia.

Tim Meyer

Meyer ameeleza kwamba hatua zilizochukuliwa na zinazoendelea kuchukuliwa kwa ajili ya kupambana na Corona soka linaweza tena kuanza kuchezwa. Kauli hiyo ya mwenyekiti wa matibabu wa UEFA inakinzana na ile kauli ya mwenyekiti wa kamati ya matibabu ya FIFA Michel D’Hooge aliyotoa siku ya Jumanne akisema kuwa mpira wa miguu haupaswi kuchezwa kwa sasa angalau hadi mwishoni mwa mwezi wa nane au mwanzoni mwa mwezi wa tisa ili kuzuia kuenea kwa maambukizi mapya ya Virusi vya Corona.

Mjumbe wa kamati kuu wa UEFA Lars-Christer Olsson


Wakati huohuo mjumbe wa kamati kuu ya UEFA Lars-Christer Olsson ambaye pia ni rahisi wa Ligi ya Ulaya amesema janga la virusi vya Corona litaharibu kalenda ya soka la Kimataifa na itaathirika kwa zaidi ya miaka miwili mpaka mitatu. Lars Olsson amesema kuwa kesi ya kusubiri na kutathimini janga la Corona ni pamoja na kuangalia michuano ijayo ya Kombe la Dunia ambayo itafanyika nchini Qatar 2022.

Olsonn amesisitiza pia lazima ufanyike mpango mbadala wa kurekebisha madirisha ya Kimataifa ya majira ya kiangazi na kuangalia uwezekano wa kurekebisha ratiba ya kufuzu kwa michuano ijayo ya Kombe la Ulaya maarufu kama Euro.

25 Komentara

    Ni bora wangesubiri mpaka kuhakikisha ugonjwa umeisha wote pande za dunia maana wachezaji wanatoka pande mbalimbali za dunia

    Jibu

    good information thanks Meridian

    Jibu

    Ni kitu Cha msingi ligi kurudi watu waendelee kupata burudani

    Jibu

    Corona imeharibu mambo mengi. Shukrani meridian kutuletea habari hii

    Jibu

    Ni wazo zuri.

    Jibu

    Wasubir mpaka corona iishe kwanza

    Jibu

    Hii habari mzuri sanaaa Asante meridian kwa taarifaa hii

    Jibu

    Corona inatufanya tusi make mkwanja

    Jibu

    Asante meridian mana ugonjwa huu no wakutisha .hii njia mliotuletea in mnzuri sana

    Jibu

    Wasubiri Corona iishe af wajipange upya…

    Jibu

    Ligi isubiri mpaka Hali itulie kabisa kwa usalama

    Jibu

    Warudishe ligi Ila kwa mashalti ya ktokuwa na mshabiki ili burudani iendelee

    Jibu

    Tunashuru kwa ujumbe meridian ila wasubiri corona iishe

    Jibu

    ligi zirudi lkn kusiwepo mashabik

    Jibu

    Hawapaswi kukinzana wanatakiwa wawe wamoja ili soka lisonge mbele

    Jibu

    Thank you Meridianbet for keeping us updated!!!!!

    Jibu

    Wasubir Kwanza huu ugonjwa wa corona upite ili muendelezo wa ligi uendelee

    Jibu

    Wazo zuri ila kwakipindi iki Cha cov19 uvumilivu uwepo

    Jibu

    Me naonelea tusubiri mpaka ugonjwa uishe kabisa ili tuwe na uwakika kwenye michezo kwa usalama wa wachezaji wetu.

    Jibu

    Korona imealibu mambo mengi

    Jibu

    @Tim Meyer mechi zirudi hata kukiwa hamna mashabiki kuanzia kama June hivi

    Jibu

    If only we could get Champions League back soon

    Jibu

    Corona imetuharibia kilakitu

    Jibu

    Kwel hayo nimaamuzi sahihi

    Jibu

    Jamanii corona imetutishia maisha

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.