Paulo Dybala amepima na kukutwa na virusi vya ugonjwa wa Corona kwa mara ya nne katika wiki sita, kulingana na ripoti. Mshambuliaji huyo wa Juventus alithibitishwa mnamo Machi 21 kuwa yeye na mpenzi wake, Oriana Sabatini walikuwa wameambukizwa COVID-19 baada ya vipimo vya kwanza vya ugonjwa huo.
Dybala amechukuliwa vipimo vinne katika wiki sita na bado yupo vile vile sawa na utambuzi wake wa kwanza. Nyota huyo kimataifa wa Argentina alizungumza hivi karibuni juu ya kupigana na ugonjwa huo, na kuelezea jinsi alivyokuwa akipata taabu kupumua.

“Kwa bahati nzuri tuko vizuri, siku hizi hatuna dalili yoyote,” alisema Dybala. “Nilikuwa na dalili zilizonimaliza nguvu, nilichoka haraka sana, wakati ninataka kufanya mazoezi, nilikuwa na pumzi kidogo baada ya dakika tano… Hapo ndipo tuligundua kuwa kuna kitu hakikuwa sawa na kupitia vipimo vya klabu yetu viliambiwa kwamba tulikuwa na COVID-19”.
Dybala alikuwa mmoja wa nyota watatu wa Juve kukutwa na coronavirus baada ya Dani Rugani na Blaise Matuidi kuthibitishwa kesi. Waziri Mkuu wa Italia Giuseppe Conte alisema wachezaji wataweza “kufanya mazoezi binafsi kutoka Mei 4, kwa vikundi kutoka Mei 18, kisha tutatathmini ikiwa kuna masharti ya kuruhusu msimu kukamilika.” Hivi Sasa Haijulikani ikiwa taarifa hii ya hivi karibuni kwa Dybala itaathiri uamuzi huu.


Samira
Get well soon champs
Furaha
Tumuombee mungu apone haraka aungane na machampion wengine
Amani macha
Inabidi azingatie mashariti ili aweze kupona kabisa
Aziza moshi
Mungu ambariki alone haraka
JULIANA
Da! Pole yake,Mungu amponye haraka
George
mambo yatakuwa sawa
Asia abdy
Afya kwanza Mungu akusaidie
povel
dah jembe letu ila mungu atampa wepesi atapona tu
Aziza moshi
Mungu ambariki apone haraka.
aisha
pole sana dybala
Ester jackson
Pole kijana