Suarez Kutua Atletico Madrid.


Barcelona wamekubali kumwachilia mshambuliaji Luis Suarez ajiunge na washindani wakuu katika Ligi Kuu ya Uhispania (La Liga), Atletico Madrid.

Suarez hatakikani kabisa kambini mwa Barcelona ambao kwa sasa wanatiwa makali na kocha mpya Ronald Koeman.

Miamba hao wa soka ya Uhispania walikuwa radhi kumwachilia Suarez ambaye ni raia wa Uruguay kujiunga na kikosi chochote bila ada ilmradi klabu ambayo angejiunga nayo si ya La Liga.

 

Suarez Kutua Atletico Madrid.

Suarez alihiari kupunguziwa mshahara ili kuingia katika sajili rasmi ya Atletico baada ya uhamisho wake hadi Juventus ya Italia kugongwa mwamba kwa sababu ya changamoto za kutafuta pasipoti na kibali cha kufanyia kazi Italia.

Rais wa Barcelona, Josep Maria Bartomeu alizuia uhamisho wa Suarez hadi Atletico kwa sababu hakutaka nyota huyo auzwe kwa kikosi ambacho ni washindani wao wakuu ligini.

Hata hivyo, baada ya kukutana na wawakilishi wa Suarez, vinara wa Barcelona waliafikiana nao baada ya fowadi huyo wa zamani wa Liverpool kufichua mipango ya kuanika kwenye vyombo vya habari jinsi “anavyohangaishwa” na Barcelona.

Atletico kwa sasa wameweka mezani kima cha Sh448 milioni kwa minajili ya huduma za Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 33.

 

Suarez Kutua Atletico Madrid.

Hata hivyo, fedha hizo huenda zikaongezeka kutegemea jinsi atakavyowajibishwa na Atletico na iwapo ataongoza kikosi hicho cha kocha Diego Simeone kupiga hatua zaidi kwenye soka ya Klabu Bingwa Ulaya (UEFA).

Uhamisho wa Suarez unatamatisha kipindi cha miaka sita ya usogora wake kambini mwa Barcelona ambao amewafungia jumla ya mabao 198 kutokana na mechi 283.

Katika enzi za ubora wake, Suarez alishirikiana vilivyo na Lionel Messi na Neymar muungano wao almaarufu MSN ukawa tishio zaidi kwa mabeki wa kikosi chochote duniani.

Mshambuliaji huyo alijiunga na Barcelona mnamo 2014 baada ya kuagana na Liverpool kwa kima cha Sh10.3 bilioni. Tangu wakati huo, ameshindia Barcelona mataji manne ya La Liga, manne ya Copa del Rey, moja la UEFA na jingine la Kombe la Dunia mnamo 2015.


FURAHIA KASINO YA MTANDAONI

Tembelea ardhi ya maajabu ushangazwe na mengi ikiwa ni pamoja na urahisi wa kujipatia utajiri kupitia Kasino ya Meridianbet.

Cheza Sasa

39 Komentara

    Kila la heri Suarez Barcelona wabinafsi sana wameona wakuachie huko ambako hakuna upizani mana wanajua moto wako

    Jibu

    piga kazi suarez nakuaminia unaga kazi mbovu ukiwa uwanjani

    Jibu

    Kila la kheri suarez

    Jibu

    Kapige kazi suarez Madrid wamekuamini

    Jibu

    Kipenda roho ula nyama mbichi

    Jibu

    Safi sana kama Suarez akienda huko

    Jibu

    Itakuwa powah snaa kma hataenda kubadilisha upepo!!

    Jibu

    Vizuri Sana suarez kapige kazi

    Jibu

    Piga kaz kijana.

    Jibu

    Kweli ni wakati mgumu na maamuzi magumu sana kwa Barca, Kila la heri Suarez

    Jibu

    Barcelona kazi wanayo mbona…

    Jibu

    Kila kheri

    Jibu

    Suarez Mambo ya shajipa

    Jibu

    Suarez kila la kheri

    Jibu

    Kila la kheri

    Jibu

    Kapige kazi broo suarez kila la kher huko uendako

    Jibu

    Asnt kwa taarif

    Jibu

    Kazi popote

    Jibu

    Kila la khery suarez

    Jibu

    Bora tu suarez alivyopata nafasi huko atletico

    Jibu

    Kila la kheri Suarez

    Jibu

    Kapige kazi suarez Madrid wamekuamini

    Jibu

    Safi piga Moira mzeee

    Jibu

    Kila la kheri

    Jibu

    Safi sana

    Jibu

    Hatimaye katua hapo

    Jibu

    Pale A.madrid atafunga sana

    Jibu

    Kila la kheri

    Jibu

    Sio mbaya

    Jibu

    Safi sana

    Jibu

    Kila la kheri

    Jibu

    Safi sana 👍

    Jibu

    Safi sanaaa

    Jibu

    Si zani kama Suarez hatabaki atletico kwa miaka yake yote hatakua kwa mda tu ili kutimiza malengo yake yakutoka Barcelona

    Jibu

    Suarez yuko vizuri!!

    Jibu

    All ze best

    Jibu

    Safi pia kubadii upepo

    Jibu

    Uhamisho wa Suarez unatamatisha kipindi cha miaka sita ya usogora wake kambini mwa Barcelona ambao amewafungia jumla ya mabao 198 kutokana na mechi 283.

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.