Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Shaaban Iddi Chilunda anatarajiwa kusaini mkataba wa kujiunga na Mouloudia Oujda ya Ligi Kuu ya Morocco.
Azam FC leo imesema kwamba imefikia makubaliano ya kumuacha mchezaji wake huyo aende Mouloudia D’oujda kukamilisha taratibu za mwisho za kujiunga na miamba hiyo ya soka Morocco.
Akijiunga na klabu hiyo, Chilunda atakuwa mchezaji wa tatu wa Kitanzania katika ligi ya Morocco baada ya beki wa kushoto, Nickson Kibabage na viungo Simon Msuva wote wanachezea Difaa Hassan El Jadida na Maka Edward wa Moghreb Tetouan.

Msuva mwenye umri wa miaka 26 sasa, ndiye aliyefungua mlango wa Watanzania katika Ligi ya Morocco baada ya kujiunga na Difaa El Jadida mwaka 2017 akitokea Yanga ya Dar es Salaam, akafuatiwa na Kibabage kutoka Mtibwa Sugar mwaka jana na Maka aliyetokea Yanga pia mwaka jana.
Chilunda aliibukia katika tmu ya vijana ya Azam FC mwaka 2012 kabla ya kucheza mechi yake ya kwanza timu ya wakubwa mwaka 2016 na Agosti 7 mwaka 2018 akajiunga na CD Tenerife ya Hispania katika Segunda División (Daraja la Kwanza) kwa mkataba wa miaka miwili.

Lakini mambo hayakumuendea vizuri huko, akatolewa kwa mkopo kwenda CD Izarra ya Segunda División B (Daraja la Tatu) kabla ya kurejea Azam FC mwaka huu.
Beti kwa Kitochi Kushinda 300,000,000!
Unajua kuwa unaweza kushinda milioni mia tatu kwa buku tu? Ndiyo! Unaweza kushinda kwa kupiga *149*10# na kubashiri. Ingia mchezoni!


Povel
Kila la kheri deal hlo litakamilik kwa chilunda
Hopemwaikuka
All ze best
Amiri Kayera
All the best chilunda
Mariam mtandama
Habari njema
Fatuma kasomo
Habari njema
Issa
Sokq la bongo linazidi kukua na kujitangaza kimataifa
Rehema
Habari njema
Saupha mohamed
Good news
Elika
Tanzania sasa tuko vizuri..pongez kwake
Neema
Habarii njema
Gabriel
Chilunda yuko vzur sana 👍
Janeflora malisa
Safi
Sauda
Maisha popote.
Fatina mfigi
Safi kijan kapige kazi
Mwajumah
Chilunda yupo vizuri sana ongera zake
Lydia Emmanuel Magoti
Vizuri Sana Chilunda piga kazi kambi kokote kijana
Caroline
Keep it up Chilunda
Zeiyana
Kila la kheri chilunda
Angelina
Safi
Ernest
Deal zuri kwa Chilunda na Azam pia
Venerose
Kapige kazi kijana
Shani
Kazi njema
aisha
Tanzania naona soka letu litafika mbali
Mariam mtandama
Safi
Fatuma kasomo
Kila la heri
Theckla
Iko poa
Asia Abdy
Apambanee
Dorophina
Kila lakheri chilunda
felister
dili zuri
magdalena
kambi popote kikubwa pesa tu nenda kijana na kila la kheri
Rose kapinga
Kazi nzuri
Sabrina
Itakua poa sana kama dili likitiki
David Pere
Good news kwa watanzaniaa
Juliana Alex
Kambi popote