Leo hii kuna gemu kali ambayo ni mechi ya Fainali ya kuwania Kombe la FA. Gemu hii ni kati ya mahasimu wawili wakongwe Chelsea na Manchester United wote wa huko Uingereza.
Katika gemu hii mjane wa Ray Wilkins, Jackie atakabidhi Kombe hilo kwa washindi huko Wembley dimbani.
Marehemu Ray Wilkins alifariki mwezi uliopita akiwa na umri wa miaka 61 ambapo alishinda Kombe la FA kama mchezaji wa Manchester United mwaka 1983 na kufunga wakati wa Fainali na pia alishinda kombe hilo mara 3 akiwa meneja wa Chelsea ambayo leo inaumana na Man United.



Povel tz
Game ngumu sana