Wachezaji washambuliaji akina Lionel Messi, Sergio Aguero, Paulo Dybala na Gonzalo Higuain wametajwa kwenye kikosi cha wasakata kabumbu 23 ambao wataiwakilisha nchi ya Argentina katika michuano ya kuwania Kombe la Dunia mwaka huu.
Icardi nje
Katika kikosi hicho mfungaji bora zaidi wa ligi ya Serie A mshambuliaji wa Inter Milan, Mauro Icardi ametupwa nje na hatokuwepo huku Aguero akijiunga na wachezaji wengine watano wa Premier League akiwemo Nicolas Otamendi wanayekipiga pamoja pale Manchester City.
Ratiba yao
Nchi ya Argentina itaanza mechi za Kombe Dunia dhidi ya Iceland tarehe 16 Juni kabla ya mechi zingine dhidi ya Croatia na Nigeria kwenye Kundi D ambapo kikosi kamili cha Argentina ni hiki hapa:
Walinda lango: Sergio Romero (Manchester United), Willy Caballero (Chelsea), Franco Armani (River Plate).
Walinzi: Gabriel Mercado (Sevilla), Federico Fazio (Roma), Nicolas Otamendi (Manchester City), Marcos Rojo (Manchester United), Nicolas Taglafico (Ajax), Javier Mascherano (Hebei Fortune), Marcos Acuna (Sporting Lisbon), Cristian Ansaldi (Torino).
Viungo wa kati: Ever Banega (Sevilla), Lucas Biglia (AC Milan), Angel Di Maria, Giovani Lo Celso (wote wa Paris St-Germain), Manuel Lanzini (West Ham), Cristian Pavon (Boca Juniors), Maximiliano Meza (Independiente), Eduardo Salvio (Benfica).
Washambuliaji: Lionel Messi (Barcelona), Gonzalo Higuain, Paulo Dybala (both Juventus), Sergio Aguero (Manchester City).



Hope mwaikuka
Axante kwa habar