Klabu ya Crystal Palace imeendelea kujiboresha kuelekea msimu ujao baada ya kumalizana na beki wa kati wa Chelsea Marc Guehi kwa kandarasi ya muda mrefu.
Guehi anatarajiwa kufanya vipimo vya afya tayari kujiunga na vijana wa Palace walio chini ya kocha mpya Patrick Vieira.
Taarifa rasmi zinasema kuwa thamani ya mchezaji ni kati ya pauni milion 15 na pauni milioni 20. Kulikuwa na klabu nyingi zilizohitaji saini ya mchezaji huyo kinda mwenye miaka 21 lakini ni Crystal Palace ndio waliofaidi.
Katika mkataba aliosaini Guehi utaisaidia Chelsea kupata kiwango cha pesa endapo mchezaji huyo atauzwa kuelekea kwenye klabu yeyote kubwa.
Crystal Palace wameendelea kuboresha kikosi chao baada ya hivi karibuni kumsajili mchezaji Michael Olise kutoka Reading na Kipa Remi Matthews siku za mwanzon za Patrick Vieira akianza kazi kama kocha mkuu klabuni hapo.
Ndio, kama bado hujajiunga na Familia ya Mabingwa ya Meridianbet, huu ndio wakati wako! Tunakupatia Bonasi ya 3,500 Tsh papo hapo kama sehemu ya ukaribisho!



dorophina
Nice update