Meneja wa Liverpool, Jurgen Klopp amethibitisha kuwa klabu hiyo imefungua mazungumzo na Mo Salah juu ya mkataba mpya wa muda mrefu.

Mkataba wa sasa wa Salah, uliosainiwa mnamo 2018, umebaki chini ya miaka miwili, lakini vyanzo vya Liverpool vina hakika makubaliano yatafikiwa, na kwamba mchezaji huyo wa miaka 29 baada ya Trent Alexander-Arnold, Fabinho, Alisson Becker na Virgil van Dijk.
Akiongea kuelekea mchezo dhidi ya Burnley, Klopp alisema: “Ninahusika katika kila kitu kinachotokea kwenye klabu. Labda mazungumzo mengine hufanyika bila mimi, hiyo inawezekana lakini sina uhakika. Mbali na hayo najua juu ya vitu vyote.
“Ni jinsi ilivyo siku zote; hatuzungumzii juu ya vitu hivi. Najua tulibadilisha hilo kidogo na Hendo [Jordan Henderson], lakini hiyo haimaanishi kwamba kuanzia sasa tutawaambia juu ya kila hatua ndogo na mazungumzo.
“Ni kweli, ikiwa imesalia miaka miwili kwenye mkataba wake unaweza kuhisi kuna mazungumzo, ipo hivyo.”
Ni muda wa kuwa milionea na kasino za mtandaoni za meridianbet, mchezo wa Sahara Riches unakupa nafasi ya kushinda mkwanja mrefu. Matajiri wa jangwani wanataka wakupe mkwanja leo.



Sarah
Jambo zuri