Tuchel : Kante ni Mchezaji Bora na Kipekee.

 

Kocha wa Chelsea, Thomas Tuchel amemtaja kiungo N’Golo Kante kama mchezaji aliyeleta mabadiliko katika ushindi wa 3-0 dhidi ya Tottenham siku ya jana [Jumapili].

 

Kante alitokea benchi kuchukua nafasi ya Mason Mount katika kipindi cha pili cha dabi hiyo ya London na kuisaidia Blues kuibuka na alama 3 muhimu.

Kante aliifungia timu yake bao la pili la mchezo na kumvutia kocha huyo wa Ujerumani na uchezaji wake katika mchezo.

“Alicheza kwa sehemu kubwa. N’Golo ni N’Golo, ni wa kipekee, wa aina yake na kuwa naye uwanjani hufanya tofauti kubwa kwa kila kitu,” Tuchel aliiambia BBC.

 

Aliongeza katika mkutano huo na waandishi wa habari: “[N’Golo] Ni mchezaji bora. Ukiwa na N’Golo, una kitu kila mtu anatafuta.

“Ni mtu wa kipekee … ni mzuri.” aliongeza Tuchel.


FUNGA BAHATI YAKO NA MERIDIANBET.

Ni wakati wa ushindi mkubwa ukiwa na kasino bomba ya Lock a Luck, meridianbet wanakupa sababu ya ushindi, funga bahati yako ya ushindi ukiwa na mabingwa.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.