Taarifa Mbalimbali za Vilabu na Mikataba

Pamoja na kwamba ligi ya Uingereza ina mvuto wa pekee lakini haimaanishi kwamba klabu hizo zinaweza kuvumilia kukaa na wachezaji kwa kipindi kirefu. Kila klabu huamua kukaa na mchezaji fulani kulingana na malengo yao na mifumo yao inayomwongoza mwalimu katika falsafa zake. Hivyo ndivyo mpira wa miguu unavyoongozwa siku zote duniani.

Klabu sita za juu bado zinaendeleza ubabe wao hata ukiangalia tofauti ya alama iliyopo kati ya United aliye nafasi ya sta kwa sasa na Watford ambaye anashika nafasi ya saba kwenye ligi hiyo. Kuna tofauti kubwa sana ya alama kati yao. Lakini hakuna lisilowezekana katika mpira wa miguu, klabu kubwa zinazoongoza na kushika nafasi hizo sa juu zinapaswa kuwa imara kwa vikosi hivyohivyo ili kujizatiti zaidi kwenye nafasi zao hizo, kinyume na hapo mambo yatakuwa tofauti.

Arsenal, wastani wa mikataba ya wachezaji kuisha kwa kikosi chao ni 2021, hii inatokana na  wachezaji kama Aaron Ramsey, Danny Welbeck, Nacho Monreal, Petr Cech, David Ospina na Stephan Lichtsteiner ambao mikataba yao inaisha mwaka huu 2019; Carl Jenkinson na Laurent Koscielny wao mikataba yao inaisha 2020; Sokratis, Mesut Ozil, Henrikh Mkhitaryan, Pierre-Emerick Aubameyang na Shkodran Mustafi wao mikataba yao inaisha 2021; Alexandre Lacazette, Sead Kolasinac, Emiliano Martínez, Mohamed Elneny, Alex Iwobi na Mattéo Guendouzi hawa mikataba yao inaisha 2022; Bernd Leno, Granit Xhaka, Hector Bellerin, Rob Holding, Ainsley Maitland-Niles, Lucas Torreira na Konstantinos Mavropanos hawa bado wana maisha marefu mikataba yao inaisha 2023.

Manchester United wao wastani wa mikataba ya wachezaji ni 2021, ambapo Ashley Young, Antonio Valencia, Juan Mata, Matteo Darmian, Ander Herrera, Phil Jones, Anthony Martial and Andreas Pereira mikataba yao inaisha mwaka huu; David de Gea, Lee Grant, Marouane Fellaini, Nemanja Matic, Marcus Rashford na Eric Bailly mikataba yao inaisha 2020; Sergio Romero, Marcos Rojo, Paul Pogba, Jesse Lingard, Victor Lindelof na Joel Pereira mikataba yao inaisha 2021; Alexis Sanchez, Romelu Lukaku na Chris Smalling hawa ni 2022 na Luke Shaw, Fred, Scott McTominay na Diogo Dalot mikataba yao inaisha 2023.

Chelsea wao wastani wa mikataba ya kikosi chao ni 2021 wachezaji kama Robert Green, Willy Caballero, Gary Cahill, David Luiz, Mateo Kovacic, Olivier Giroud na Lucas Piazon mikataba yao itaisha 2019 hii; Eden Hazard, Willian, Pedro, Marco van Ginkel na Callum Hudson-Odoi wastani wa mikataba ni 2020; Jamal Blackman, Davide Zappacosta na Ruben Loftus-Cheek mikataba yao inaisha 2021; Cesar Azpilicueta, Danny Drinkwater, Antonio Rudiger, Alvaro Morata, Emerson na Andreas Christensen mikatava yao inaisha 2022; Jorginho, Marcos Alonso, Ross Barkley, N’Golo Kante na Ethan Ampadu wao mikataba yao inaisha 2023 na Kepa Arrizabalaga ambaye bado ana maisha marefu hapo hadi 2025. Hizo ni baadhi ya klabu kubwa ambazo zipo hatarini kupoteza wachezaji wao wakubwa.

3 Komentara

    Mmh noma

    Jibu

    Taarifa njema

    Jibu

    Mambo ni moto

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.