Meneja wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer amesifu uwezo wa mshambuliaji wake Cristiano Ronaldo na kumfananisha na lejendari wa mpira wa kikapu, Michael Jordan.

Solskjaer amesema Ronado anaipa Man United ubora sawa na ambao lejendi wa kikapu Michael Jordan alikuwa anawapa timu ya Chicago Bulls baada ya sare ya jana dhidi ya Atalanta.
Ronaldo alifanikiwa kufunga magoli mawili na kuisaidia Man United kupata alama moja ugenini baada ya Atalanta kuongoza mara mbili mfululizo dhidi ya wageni wao.
Ronaldo, 36 amefanikiwa kufunga magoli ya kuwarudisha mchezoni Man United katika michezo miwili ya ligi ya mabingwa, dhidi ya Villarreal na Atalanta.
“Kila mtu ana kazi na majukumu yake,” Solskjaer aliwaambia waandishi wa habari “Ronaldo ni kiongozi wa timu lakini kile ndio anachofanya, anafunga magoli.
“Hatujafurahishwa kuruhusu magoli mawili, lakini ametupa wakati na nina uhakika Chicago Bulls hawakujali kuwa na Michael Jordan pia.” aliongeza Soskjaer.
Mkwanja umetema ndani ya kasino za meridianbettz, Mchezo maridhawa wa Aurora Beast Hunter unakupa nafasi sawa ya ushindi leo hii, kila mzunguko una nafasi ya kuibuka mshindi, na mkwanja wako unaupata kila mzunguko utakapo kamilika.


