Unai Emery Achagua Kusalia Villarreal

Kocha mkuu wa klabu ya villarreal Unai Emery ameikataa offa iliyotolewa na klabu ya Newcastle ya kuhitaji huduma yake badala yake amechagua kubaki kwenye klabu yake ya sasa Villarreal

Kocha huyo mwenye umri wa miaka 50 alithibitisha hilo baada ya mchezo wake wa ligi ya mabingwa na young boys ambao Villarreal ilishinda 2-0.

 

Pia Unai Emery alipost kwenye kwenye mtandao wa Twitter akisema, “Villarreal ni nyumbani na nimejizatiti hapa, kiukweli nafurahi kusikia klabu bado inavutiwa na mimi lakini zaidi ya mimi kuwa hapa.”

“Ndiyo maana nimeongea na mmiliki wa klabu, raisi Fernando Roig maamuzi yangu ya kutaka kuendelea na mradi huu, kwasababu ya kujitoa kwao na heshima ninayopata kutoka kwenye klabu na wachezaji hapa.”

“Ingawa kulikuwa na tetesi jana kutoka nchi nyingine, ndani ya klabu kulikuwa na uwazi na uaminifu, kwa familia ya Roig na wafanyakazi kwa ujumla, kwangu mimi ni kitu muhimu sana, Villarreal ni nyumbani na najitoa kwa asilimia 100.”

Newcastle ilimfuta kazi kocha wake Steve Bruce mapema baada ya matajiri wapya kununua klabu hiyo baada ya muendelezo mbovu aliokuwa nao baada ya kushika nafasi ya 19 kwenye michezo 10 huku akivuna pointi 4, kwa sasa Newcastle inaongozwa na kocha wa muda Graeme Jones huku wakitafuta mrithi wake.


MKWANJA WA KUSHATO NA AURORA BEAST HUNTER!

Mkwanja umetema ndani ya kasino za meridianbettz, Mchezo maridhawa wa Aurora Beast Hunter unakupa nafasi sawa ya ushindi leo hii, kila mzunguko una nafasi ya kuibuka mshindi, na mkwanja wako unaupata kila mzunguko utakapo kamilika.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.