Kiungo mkata umeme wa klabu ya Yanga SC, Khalid aucho ameweka wazi historia yake mpaka kutua katika ligi ya NPL, huku akisema hajawahi kuzungumza na kiongozi yoyote wa Simba SC.
βNilikuwa nasikia uvumi kwamba nilikuwa natakiwa pia na Simba SC kuwa nakwenda Simba, ukweli ni kwamba sikuwa na ofa yoyote na Simba na wala hakuna kiongozi wao ambaye alinipigia mimi na nikaongea nao.” alianza Aucho.
“Ukweli ni kwamba nilikuwa na ofa mbili tu Tanzania nilikuwaa nahitajika na Azam, niliongea nao na tukafikia sehemu lakini ya pili ni Injinia (Hersi Said) huyu ndiye niliyeongea naye sana na nikaona mambo yanakwenda sawa na mwisho tukakubaliana na nikaja kusaini hapa Yanga.
“Uamuzi wangu wa kuja Yanga SC ulitokana na kuhitaji changamoto mpya ambayo niliiona hapa patakuwa sehemu sahihi kwangu.” aliongeza.
Aucho mpaka sasa ameisaidia klabu yake kushinda mechi tano wakiwa hawajapoteza mchezo wowote, wamefunga magoli tisa na kufungwa goli moja pekee tangu msimu uanze.
Mkwanja umetema ndani ya kasino za meridianbettz, Mchezo maridhawa wa Aurora Beast Hunter unakupa nafasi sawa ya ushindi leo hii, kila mzunguko una nafasi ya kuibuka mshindi, na mkwanja wako unaupata kila mzunguko utakapo kamilika.