Varane Apata Majeraha Dhidi ya Atalanta.

 

Beki wa Manchester United, Rafael Varane amepata majeraha katika mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Atalanta uliopigwa siku ya jana, Meneja Ole Gunnar Solskjaer amesikitishwa na majeraha hayo.

 

Solskjaer ameweka wazi Varane amepata majeraha ya nyama za paja na si mazuri kwa jinsi tatizo linavyoonekana baada ya kulazimika kutolewa katika kipindi cha kwanza katika mchezo wa jana.

“Alijisikia nyama za paja zinavuta, itabidi tumfanyie uchunguzi kesho. Lakini alijiskia maumivu ya nyama za paja alipokuwa anakimbia. Hakuhitaji kujiweka katika matatizo zaidi. Uchunguzi wa kwanza haukuwa mzuri lakini atafanyiwa uchunguzi tena kesho.”

Varane amefanikiwa kucheza michezo 6 tangu ajiunge na Man United akitokea Real Madrid huku akipata majeraha kwa mara ya pili mfululizo tangu alipojiunga na ligi kuu ya uingereza.


MKWANJA WA KUSHATO NA AURORA BEAST HUNTER!

Mkwanja umetema ndani ya kasino za meridianbettz, Mchezo maridhawa wa Aurora Beast Hunter unakupa nafasi sawa ya ushindi leo hii, kila mzunguko una nafasi ya kuibuka mshindi, na mkwanja wako unaupata kila mzunguko utakapo kamilika.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.