Simba SC Kuwavaa Namungo Leo.

 

Kikosi cha Simba SC kitaingia uwanjani leo kupambania alama tatu muhimu kutoka kwa Namungo FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC utakaopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa majira ya saa moja usiku.

Kocha Msaidizi wa Simba SC, Seleman Matola, amesema kwa sasa wanapitia kipindi kigumu wachezaji wanacheza kwa presha kubwa lakini benchi la ufundi linashughulikia kuwarejesha katika hali zao.

Matola amesema morali ya wachezaji ipo juu na kila mmoja yupo tayari kwa ajili ya kupambana kuhakikisha tunawapa furaha Wanasimba leo.

 

“Tunapitia kipindi kigumu, wachezaji wanacheza kwa presha ndiyo maana tunapoteza nafasi nyingi lakini tunaendelea kulifanyia kazi na kuelekea mechi ya leo kutakuwa na mabadiliko makubwa,” amesema Matola.

Kuelekea mchezo wa leo Simba SC itakosa huduma ya wachezaji wake watano ambao ni majeruhi huku mmoja akitumikia adhabu ya kadi nyekundu.

Wachezaji wa Simba SC ambao ni majeruhi ni Chris Mugalu, Pape Ousmane Sakho, Taddeo Lwanga, Sadio Kanoute na Mzamiru Yassin.

Mlinzi wa kati Henock Inonga Baka nae atakosekana kwenye mchezo wa leo na mechi nyingine mbili zijazo za ligi kutokana na kutumikia adhabu ya kadi nyekundu.


MKWANJA WA KUSHATO NA AURORA BEAST HUNTER!

Mkwanja umetema ndani ya kasino za meridianbettz, Mchezo maridhawa wa Aurora Beast Hunter unakupa nafasi sawa ya ushindi leo hii, kila mzunguko una nafasi ya kuibuka mshindi, na mkwanja wako unaupata kila mzunguko utakapo kamilika.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.