Tetesi za Soka Barani Ulaya.

 

Tetesi zinasema, Mshambuliaji wa England Harry Kane, 28, ataachana na mipango ya kuondoka Tottenham baada ya kuwasili kwa Antonio Conte kuifundisha klabu hiyo.

Tetesi zinasema, Conte anajiandaa kwa usajii wa kwanza wa kiungo wa kati wa AC Milan Franck Kessie na Stefan de Vrij kutoka Inter Milan akiwa kocha wa Tottenham.

Paul Pogba wa Manchester United anapendelea kurejea Juventus badala ya kujiunga na Paris St-Germain au Real Madrid wakati kiungo huyo wa kati wa Ufaransa, 28, atakapokuwa mchezaji huru msimu ujao.

 

Man United

Tetesi zinasema, Erling Braut Haaland ameamua kuondoka Borussia Dortmund na wakala wake anataka mshambuliaji huyo wa Norway, 21, ajiunge na Barcelona.

Mshambuliaji wa Real Madrid, Eden Hazard anaweza kujiunga na Newcastle wakati wa dirisha la usajili mwezi Januari, huku Carlo Ancelotti akijiandaa kumuachia Mbelgiji huyo, 30.

Newcastle wanapanga uhamisho wa huru kwa mchezaji wa Inter Milan Marcelo Brozovic huku kiungo mkabaji wa Croatia, 28, akimaliza mkataba wake msimu ujao.

Licha ya Unai Emery kuwa na nafasi zaidi, kocha wa Ubelgiji Roberto Martinez anatazamiwa kubeba mikoba ya kocha wa Newcastle na kocha wa muda Graeme Jones, ambaye hapo awali alikuwa msaidizi wa Mhispania huyo akiwa Ubelgiji.

Tottenham, West Ham na Southampton zinamfukuzia mlinda mlango wa West Brom Sam Johnstone,28, ambaye mkataba wake utakwisha majira yajayo ya joto.

 

Tetesi zinasema, Tottenham wako tayari kuchuana na Juventus kumnasa mshambuliaji wa Fiorentina, Mserbia Dusan Vlahovic,21.

Christian Eriksen yuko tayari kujiunga tena na Ajax mnamo Januari kwani kiungo huyo wa kati wa Denmark, 29, hawezi kuichezea klabu yake ya sasa ya Inter Milan akiwa amewekewa kifaa cha moyo cha kudhibiti mapigo ya moyo.

Kiungo wa Fabio Carvalho amekataa ofa kubwa ya kusalia Fulham huku winga huyo mwenye umri wa miaka 19, ambaye amekuwa akihusishwa na Real Madrid, sasa mkataba wake utamalizika mwishoni mwa msimu huu.


MKWANJA WA KUSHATO NA AURORA BEAST HUNTER!

Mkwanja umetema ndani ya kasino za meridianbettz, Mchezo maridhawa wa Aurora Beast Hunter unakupa nafasi sawa ya ushindi leo hii, kila mzunguko una nafasi ya kuibuka mshindi, na mkwanja wako unaupata kila mzunguko utakapo kamilika.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.