Klabu ya PSG wanajitahidi kwenda na kasi ya League 1 huku wakiwa wanakabiliwa na kibarua cha Ligi ya Mabingwa bila kuwa na mchezaji wao machachari, mwenye michezo ya maudhi kwa wapinzani Neymar! Thomas Tuchel ansema kuwa licha ya ukweli kuwa ‘hatuna Neymar mwingine’ lakini bado ana imani na kikosi chake kufanya poa.
Nemar anatarajiwa kukosa gemu za klabu hii kwa miezi mingine miwili Ijayo akiwa anauguza jeraha lake alilolipata kwenye gemu dhidi ya Starsbourg mwezi uliopita. Gemu ambayo mchezo wake madaha uliwaudhi wapinzani na kwa kiasi fulani ulimponza akachezewa rafu mara 3 kabla hajajiumiza mguu wake kwa kuukanyagia vibaya.

“Hatuna Neymar, Ila nawaamini wachezaji wengine”!
PSG wameweza kushinda gemu yao ya kwanza bila nyota huyu waliyocheza dhidi ya Rennes, lakini wameshindwa kwenda na moto huo huo kwenye gemu ya pili ambayo walichapwa bao 2-1 dhidi ya Lyon.
Angel Di Maria alionekana kufanya vyema na kuwapa goli la mapema PSG, lakini Mousa Dembele na Nabir Fekir wakaipatia Lyon ushindi kwa kutupia Magoli 2.
Hata hivyo, meneja wa PSG bwana Tuchel ana mtazamo chanya na kikosi chake akiamini kulikuwa na makosa ambayo yanaweza kurekebishwa na wakaweza kufanya vyema kwenye vibarua walivbyo navyo mbele yao.

