Unafikiri nani atachukua kiatu cha dhahabu kwa msimu wa mwaka 2018-2019? Messi ameendelea na rekodi nzuri ya kuchapa magoli msimu huu akifanikiwa kupachika jumla ya magoli 21 baada ya kutia nyavuni magoli yote kwenye sare dhidi ya Valencia gemu ya LaLiga Jumamosi.
Messi amemtupa Cristiano Ronaldo kwa tofauti ya magoli ma 4, Ronaldo naye alicheka na nyavu mara mbili kwenye gemu ya Serie A ambayo walitoka sare dhidi ya Parma na kufikisha idadi ya magoli 17 kwa Jumla. Ushindani zaidi ulikuwa unatarajiwa kuwa ni kati ya Ronaldo na Messi, lakini kuna vijana wengine wanaofanya poa akiwemo Kylian Mbappe.
Katika msimamo mpya wa wanaowania tuzo ya mfungaji bora wa ulaya atakayetwaa Kiatu cha Dhahabu, Lionel Messi ndiye anayeongoza akifuatiwa na Kylian Mbappe ambaye kwa sasa naye amefikisha magoli 18, tofauti ya goli moja na Ronaldo.
Orodha ya Jumla (Magoli yamezidishwa kwa viwango vya UEFA kuanzia 1-2 ili kupata pointi za jumla)
1. Lionel Messi, Barcelona: 21 x 2.0 difficulty factor = 42.0
2. Kylian Mbappe, Paris Saint-Germain: 18 x 2.0 = 36.0
3. Cristiano Ronaldo, Juventus: 17 x 2.0 = 34.0
T4. Mohamed Salah, Liverpool: 16 x 2.0 = 32.0
T4. Edinson Cavani, Paris Saint-Germain: 16 x 2.0 = 32.0
T4. Fabio Quagliarella, Sampdoria: 16 x 2.0 = 32.0
T4. Nicolas Pepe, Lille: 16 x 2.0 = 32.0
8. Liliu, Kalju: 31 goals x 1.0 = 31.0 points
T9. Mbaye Diagne, Kasimpasa: 20 x 1.5 = 30.0
T9. Zakaria Beglarishvili, Flora: 30 x 1.0 = 30.0
T9. Paulinho, Hacken: 20 x 1.5 = 30.0
T9. Luis Suarez, Barcelona: 15 x 2.0 = 30.0
T9. Duvan Zapata, Atalanta: 15 x 2.0 = 30.0
T9. Pierre-Emerick Aubameyang, Arsenal: 15 x 2.0 = 30.0

