Mpango wa Emery Umefeli Januari

Meneja wa Arsenal UNai Emery ameweka wazi kuwa mpango wake uliokuwa kwa dirisha la usajili la mwezi Januari umefeli baada ya kushindwa kufikia lengo alilokuwa nalo mezani juu ya dirisha hili.

Kwa mujibu wa meneja huyu, washika mtyutu walikuwa wanatarajia kuwasajili wachezaji watatu kwenye dirisha hili, lakini wamefanikiwa kumsajili mchezaji mmoja tu ambaye ni Denis Suarez.

“Klabu ilikuwa inajitahidi tukifanya kila tuwezalo. Tulikuwa tunatazamia kupata wachezaji watatu, lakini kama tru wangeweza kuja kwa kuendana na masharti yetu na pia kama tunaona wangeweza kutusaidia kufanya vyema zaidi ya wachezaji ambao tunao hapa” -Unai Emery

Akitaja kuwa Denis Suarez tu, ndiye mchezaji waliyefanikiwa kwenda naye sawa na kumleta klabuni hapo amebainisha kuwa dirisha la usajili linakuwa na mambo mengi ambayo wakati mwingine ni vigumu kubadilika ili kuendana nayo.

Meneja huyu anadai licha ya kufeli kwa matazamio yake na ya klabu kwa ujumla, bado anayo furaha kuwa na wachezaji alio nao kwa sasa na anaamini wanaweza kuwa na nguvu na motisha wa kutosha kukamili vibarua walivyonavyo.

“Ninafurahia wachezaji tulionao hapa. Tunawachezaji ambao bado wanarejea afya nzuri baada ya kupata majeraha na nafikiri watatusaidia kufanya vizuri zaidi.” –Emery

 

4 Komentara

    Pole sana meneja

    Jibu

    Pole utapona#meridianbett

    Jibu

    Duh majanga

    Jibu

    Duu majanga haya

    Jibu

Acha ujumbe